‘Sisikii’ ni jina la wimbo
ambao unafanya vizuri kwenye radio na TV pia, wimbo huo video yake yote
ilifanywa China, ndani yake alionekana pia video queen msanii wa Bongo
Fleva Vanessa Mdee.. Jux
karudi tena location, safari hii kazi haijafanyika China tena na wala
sio nje ya Bongo, mzigo unafanyika hapa Tz, walikuwa zao kwenye fukwe za
bahari ya Hindi Dar es Salaam wakishoot video ya wimbo mpya wa staa
huyo.
Wimbo unaitwa ‘Nikuite Nani’, tayari kazi ya kuandaa video imeanza muda wowote ikiwa tayari tutaiona, hapa nimekuwekea behind the scenes baadhi ya pichaz.. Vee Money ameonekana yuko nae kwa pembeni akicheki Jux na team ya Hanscana wakirekodi video hiyo ufukweni.
Kingine nilichokishuhudia ni kwamba
video iko simple kabisa yani, hakuna magari ya kifahari wala majumba
yaliyotumiwa kushoot, muda mwingi picha za video zimerekodiwa wako zao
tu ufukweni.
0 maoni:
Post a Comment