Vinara wa ligi kuu ya England,
Chelsea leo usiku wamejikuta wakiambulia majonzi baada ya kutolewa
katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya na Wapinzani PSG huku
wakiwa mbele ya mashabiki wao kunano Uwanja wa Stamford Bridge baada ya
kulazimishwa sare ya 2-2.
Licha ya PSG kucheza wakiwa
pungufu kwa kipindi kirefu kufatia Nyota wake Zlatan Ibrahimovic kupewa
kandi nyekundi ya moja kwa moja baada ya kumfanyia madhambi Oscar katika
dakika ya 32 kipindi cha kwanza, hawakuweza kuvunjika Moyo zaidi
waliongeza nguvu na kusaka ushindi hatimaye sasa Wametinga hatua ya Robo
fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya Vilabu.
Chelsea ndio walianza kupata bao
kupitia kwa Gary Cahill kunako dakika ya 80 kipindi cha pili kufatia
kona iliyopigwa na mabeki wa PSG wakashindwa kuosha mbele ndipo mchezaji
huyo akafumua shuti ambalo lilitinga kambani, Bila kukata tamaa
Wafaransa hao (PSG) walikomaa na kujipatia bao la kusawazisha katika
dakika ya 85 kupitia kwa David Luiz, ambapo hadi dakika 90 zinamalizika
Chelsea ilikuwa imebanwa mbavu na PSG kwa kukubali sare ya 1-1.
Kama kawaida ziliongezwa dakika
30 ili kupatikana mbabe wa mchezo, Thiago Silva beki wa PSG akanawa
mpira katika eneo la 18 na muamuzi akawazawadia Chelsea Penati ambayo
ilipigwa na Eden Hazard na kuipatia timu yake bao la 2 ikiwa ni dakia ya
95.
Lakini wahenga walisema kuwa
“Siku ya kufa nyani miti yote huteleza” Thiago Silva akisawazisha makosa
yaliyoipatia Chelsea bao la pili, Akawakata maini mashabiki na wapenzi
wa The Blues baada ya kupiga kichwa safi kufatia mpira wa kona na
kuiandikia PSG bao la kusawazisha ikiwa ni dakika ya 114 na kufanya
kibao kisomeke 2-2.
0 maoni:
Post a Comment