Mar 12, 2015

TENGA APIGA BAO ‘LAINIII’ CAF, MPINZANI WAKE AJIONDOA MWENYEWE UCHAGUZI WA APRILI 7

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Leodegar Chillah Tenga (pichani kulia) amepiga hatua moja mbele katika kuelekea kutetea nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Hiyo inafuatia aliyekuwa mpinzani wake, Rais wa Shirikisho la Soka Djibouti (DFF), Suleiman Hassan Waberi kujitoa kuwania nafasi hiyo.
Waberia ameandika barua ya kujitoa kwenye orodha ya wawania nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF kutoka Afrika Mashariki na Kati na sasa jina la Tenga pekee, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), litakwenda Cairo.
Katika barua yake, Waberi amesema amefikia hatua hiyo baada ya kupokea ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa CECAFA wakimtaka amuachie Tenga nafasi hiyo.    
Mkutano Mkuu wa 37 wa mwaka wa CAF unatarajiwa kufanyika Jumanne ya Aprili 7, mwaka huu katika ukumbi wa Marriot uliopo ndani ya hoteli ya Zamalek mjini Cairo, Misri kuanzia Saa 3: 30 asubuhi.
Barua ya Waberi kujitoa uchaguzi wa CAF

0 maoni:

Post a Comment