Mdau
maarufu wa soka nchini, Abdulfatah Saleh ameeleza hisia zake kwa
kusikitishwa na msiba ulioikumba familia ya wanamichezo na hasa wapenda
soka baada ya kuondokewa na Sylvester Marsh.
Marsh
aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars, Kilimanjaro Stars na
baadhi ya timu za Ligi Kuu Bara, amefariki leo asubuhi katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Marsh alilazwa Muhimbili wiki chache zilizopita akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya koo ambao ulikuwa ukimsumbua kwa muda sasa.
Kumbukumbu zinaonyesha mdau huyo alikuwa kati ya waliojitokeza kumsaidia Marsh kwa hali na mali wakati akiwa mgonjwa.
Abdulfatah, mmiliki
wa
Hoteli ya Sapphire Court ya Kariakoo jijini Dar es Salaam alisema msiba
wa Marsh ni sehemu ya mafunzo kwa wanamichezo kama wanadamu.
"Kila
mmoja ataonja mauti, hili ni vizuri kila mmoja kulikumbuka. Lakini
tujifunze pia kusaidiana na kupendana wakati tukiwa hai.
"Urafiki
si kufanana, ni kufaana. Vizuri mtu anapokuwa na matatizo tukamkumbuka
kwa kuwa hatujui baada ya fulani, matatizo yatahamia kwa nani," alisema
Abdulfatah akionyeshwa kuguswa na msiba wa kocha huyo aliyekuwa
akimiliki kituo cha kukuza vipaji vya watoto katika mchezo wa soka huko
Mkoani Mwanza.
Ingawa alikuwa akifanya siri kubwa huenda kwa kufuata misingi ya dini, Abdulfatah ndiye alijitolea
kumhudumia kocha huyo katika matibabu yake.
Juhudi kuhakikisha Marsh anapata matibabu bora hadi alipopata nafuu na kurejea kwao Mwanza. Lakini baada ya miezi michache baadaye alirejeshwa tena akiwa katika ambayo haikuwa nzuri hadi mauti yalipomkuta.
0 maoni:
Post a Comment