Baada ya uongozi wa Yanga kuwaomba mashabiki wa klabu
tofauti za hapa nchini kujitokeza na kuwapa sapoti kwenye mchezo wao wa kesho
Jumapili wa Kombe la Shirikisho dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe, mashabiki wa
Simba wa Tawi la Mpira na Maendeleo, maarufu kwa jina la Simba Ukawa,
wamekubali kufanya hivyo ila wakatoa masharti.
Yanga, kesho inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar, kucheza na Platinum, mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya michuano
hiyo. Ikumbukwe kuwa Yanga imetinga hatua hiyo baada ya kuiondoa BDF IX ya
Botswana, huku wapinzani wao wakiitoa Sofapaka ya Kenya.
Mwenyekiti wa tawi
hilo, Mohammed Kingolile, amesema kuwa wao linapokuja suala la klabu
kuiwakilisha nchi, huwa hawana kinyongo na Yanga, hivyo wapo tayari
kuishangilia kwa nguvu zote.
“Tupo tayari kuwashangilia lakini kauli za kuikejeli
Simba alizozitoa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu yao, Jerry
Muro, kabla ya mchezo wetu dhidi yao wiki iliyopita, zimetufanya kusita
kuishangilia mpaka pale watakapotuomba radhi.”
SOURCE: CHAMPIONI JUMAMOSI.
0 maoni:
Post a Comment