Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
BAO la Emmanuel Anord Okwi dakika ya 90 ushei limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba SC sasa inafikisha pointi 29 baada ya mechi 18 na kuendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 30 za mechi 16 sawa na vinara Yanga SC, wenye pointi 31.
Okwi alifunga bao hilo, wakati tayari baadhi ya wapenzi wa Simba SC wameanza kutoka uwanjani, wakiamni matokeo ni sare. Mganda huyo, alifunga baada ya kupata pasi ya Abdi Banda na kumchambua vizuri kipa aliyefanya kazi nzuri leo, Said Mohamed Kasarama.
Mchezo
huo uliochezeshwa na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, aliyesaidiwa
na Yussuf Sekile wa Ruvuma na Abdallah Rashid wa Pwani, Simba SC ndiyo
waliotawala na kutengeneza nafasi nyingi, lakini hawakuwa na bahati ya
mapema.
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi aliiongoza vyema safu ya ushambuliaji ya Mtibwa Sugar akisaidiana na Ame Ally, lakini wakaishia kuisumbua tu ngombe ya Simba, iliyoongozwa na beki chipukizi, Hassan Isihaka.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murushid, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Said Ndemla, Abdi Banda, Elias Maguri, Emmanuel Okwi na Simon Sserunkuma/Ramadhani Singano ‘Messi’.
Mtibwa Sugar; Said Mohammed, Said Mkopi, Dacis Luhende, Salim Mbonde, Andrew Chikupe, Shaaban Nditi, Ally Sharrif, Henry Joseph, Ame Ally/Mohammed Mkopi, Muzamil Selemba/Ally Yussuf na Mussa Hassan Mgosi/Vincent Barnabas.
BAO la Emmanuel Anord Okwi dakika ya 90 ushei limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba SC sasa inafikisha pointi 29 baada ya mechi 18 na kuendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 30 za mechi 16 sawa na vinara Yanga SC, wenye pointi 31.
Okwi alifunga bao hilo, wakati tayari baadhi ya wapenzi wa Simba SC wameanza kutoka uwanjani, wakiamni matokeo ni sare. Mganda huyo, alifunga baada ya kupata pasi ya Abdi Banda na kumchambua vizuri kipa aliyefanya kazi nzuri leo, Said Mohamed Kasarama.
Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza Okwi leo baada ya kufunga bao pekee la ushindi dakika za lala salama dhidi ya Mtibwa Sugar |
Emmenuel Okwi akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Said Mkopi katika mchezo wa leo |
Beki wa Simba SC, Hassan Kessy akimtoka kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi |
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi aliiongoza vyema safu ya ushambuliaji ya Mtibwa Sugar akisaidiana na Ame Ally, lakini wakaishia kuisumbua tu ngombe ya Simba, iliyoongozwa na beki chipukizi, Hassan Isihaka.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murushid, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Said Ndemla, Abdi Banda, Elias Maguri, Emmanuel Okwi na Simon Sserunkuma/Ramadhani Singano ‘Messi’.
Mtibwa Sugar; Said Mohammed, Said Mkopi, Dacis Luhende, Salim Mbonde, Andrew Chikupe, Shaaban Nditi, Ally Sharrif, Henry Joseph, Ame Ally/Mohammed Mkopi, Muzamil Selemba/Ally Yussuf na Mussa Hassan Mgosi/Vincent Barnabas.
0 maoni:
Post a Comment