Mmoja wa viungo wenye uwezo
wa juu ni Haruna Moshi ‘Boban’. Lakini siku hizi ameadimika na amekuwa akifanya
mazoezi binafsi.
Mmoja wa wadau wa soka na
kiongozi wa Villa Squad, Iddi Godigodi ametupia picha Boban akijaribu
kumdhibiti mshambuliaji ‘hatari’ Nassor Bin Slum.
Katika picha hiyo ya
mtandao wa kijamii aliyotupia Godigodi, inaonekana Boban akijaribu kumba Bin
Slum akiwa kwenye mwendo.
Fitness ya Bin Slum
inaonekana kuwa juu na Boban anayumba akiwa njiani kuelekea kulamba mchanga.
Walioiona picha hiyo,
maswali yao” Huyu huyu Bin Slum anayezidhamini Mbeya City, Stand United na Wana Ndanda kucheeree yuko
fiti hivi”.
Wengine: “Boban kwa ameisha
kiasi hicho?” basi kila mmoja ana swali lake.
0 maoni:
Post a Comment