Chelsea imekubali kumuuza mshambuliaji wake Andre Schurrle ili kupata ufadhili wa kumsajili Juan Cuadrado.
Hatua
hiyo ya kumsajili Cuadrado mwenye umri wa miaka 26 inaweza kukamilishwa
katika mda unaohitajika kwa yeye kuichezea Chelsea dhidi ya Mancity
siku ya jumamosi.Gazeti la Mail online limegundua kwamba makubaliano hayo ambapo takriban pauni millioni 60 zitatumika yanakaribia katika kipindi cha saa 24 zijazo.
Chelsea inamuuza Shurrle kwa kitita cha pauni millioni 30 huku kilabu ya Wolfburg ikimhitaji nayo Borussia Dortmund pia nayo ikimtaka.
Kocha Jose Mourinho hampendelei mchezaji huyo wa Ujerumani,lakini anatambua thamani yake katika soko la uhamisho.
Mshambuliaji huyo wa Ujerumani vilevile anataka kurudi nyumbani.
0 maoni:
Post a Comment