Jan 29, 2015

MASAU BWIRE ATUA OFISI ZA CHAMPIONI KUHAKIKI PICHA ZA TAMBWE KUKABWA


MHARIRI KIONGOZI WA CHAMPIONI, SALEH ALLY (KUSHOTO) AKIMUONYESHA MASAU BWIRE PICHA HALISI YA TAMBWE AKIKABWA NA GEORGE MICHAEL. KULIA NI MHARIRI WA GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO, PHILLIP NKINI.
Kuonyesha hataki mzaha, Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ametua kwenye ofisi za Gazeti namba moja kwa habari za Michezo la Championi na kutaka kuhakikisha ile picha iliyoonyesha beki George Michael akimkaba mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga.


Awali Masau aliwahi kuonyesha hofu yake kuhusiana na picha hiyo kwamba huenda ilifanyiwa utundu.

Leo akiwa katika ofisi za Global Publishers, Masau alishuhudia picha hiyo pamoja na nyingine kadhaa za mechi kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting na kumaliza ubishi.
Masau alionyeshwa picha hizo na Mhariri Kiongozi wa Gazeti la Championi pamoja na Wahariri wengine, Phillip Nkini na Ezekiel Kitula. Pia waandishi Martha Mboma, Hans Mloli na Wilbert Molandi nao walishuhudia Masau akionyeshwa picha hizo.
  "Kwa kweli mmejitahidi sana, picha nimeziona na kweli ninawpaongeza sana. Ndiyo maana nikafika hapa kumaliza ubishi," alisema Masau kabla ya kuendelea mazungumzo mengine ya kawaida kabla ya kuondoka zake.
Picha ya Tambwe akikabwa na beki huyo ilizuia utata mkubwa. Lakini siku chache baadaye naye alizungumza na kusema aling'atwa na Tambwe.

0 maoni:

Post a Comment