Jan 29, 2015

JAY MOE; NARUDI KIVINGINE MSISHANGAE MKINISIKIA KWENYE BEAT KAMA ZA AKINAASAP ROCKY AU FRENCH MONTANA

Jay moe anarudi tena. Hata hivyo ametoa onyo kwa mashabiki wake wa kitambo wasistuke sana kumsikia akirap tofauti na walivyo mzoea.
Akiongea na kipindi cha Siz kitaa kinachorushwa na clouds tv hit maker huyo wa "kama unataka demu" amedai kuwa baada ya kukaa kimya kwa miaka miwili ambapo alikuwa anafanya mambo muhimu ya kimaisha hivi karibuni atarejea tena kwenye muziki.

Raper huyo amesema mashabiki wategemee makubwa kwa sababu muziki umebadilika na yeye hajaachwa nyuma huku akisema kuwa beat aliyo itumia ni kama zile zinazofanya vizuri marekani za wasanii kama Asap rocky au French montana.

Amesema wimbo huo ametumia mtindo tofauti ambao watu wengi hawategemei kama anaweza kuifanya kwa mtindo wa kizazi cha kisasa.

Moe anadai amesharekodi wimbo mpya uitwao "Jah" alio mshirikisha Gnako.


 

0 maoni:

Post a Comment