Jan 29, 2015

PLUIJM ASEMA WATAIMARIKA KWA KUCHEZA MECHI NGUMU


PLUIJM (KUSHOTO) AKIWA NA MENEJA WA YANGA, HAFIDHI SALEH.
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kikosi chake kitakuwa kinaimarika zaidi kutokana na wanavyocheza mechi ngumu.

Pluijm raia wa Uholanzi amesema kikosi chake kina ubora wa juu lakini kuna mambo yanayotakiwa kurekebishwa.

"Ndiyo maana tunaendelea kupambana, tunafanya kazi na kila mara tunazungumza.

"Hivyo si jambo la leo pekee au kesho, tunaendelea kubadilisha na sasa nguvu nyingi iko kwa ajili ya mechi ijayo dhidi ya Ndanda FC.

"Tuna muda wa kutosha kujiandaa kabla ya mechi hiyo ya Jumapili na tuna mambo muhimu ya kubadili. Kikubwa ni kila mtu kumuamini mwenzake," alisema Pluijm.

0 maoni:

Post a Comment