Jan 29, 2015

TAMBWE: BADO HATUJAFIKIA KIWANGO TUNACHOTAKA NA HATUJAKATA TAMAA


TAMBWE(KULIA) AKIWA MAZOEZINI YANGA
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amesema licha ya kutofanya vizuri katika kiwango anachotaka yeye na wenzake, wamekuwa wakiendelea kujituma tu.



Tambwe amesema wamekuwa wakijituma kwa juhudi kubwa huku wakiamini mambo yatabadilika kama hawatakata tamaa.

"Unajua ukiendelea kujituma, hata kama hayaendi vizuri baadaye yanaweza kubadilika na ukafanya vizuri.

"Kitu kizuri mimi na wenzangu hatukati tamaa, hata ukija mazoezini utaona watu wanavyojituma na tuna imani siku itafika tuanze kufanya vizuri," alisema Tambwe.

0 maoni:

Post a Comment