KIUNGO
wa Manchester United, Juan Mata ameingia katika rada za usajili za
Barcelona kwa mwaka 2016 na tayari miamba hiyo ya Katalunya imeshaanza
mipango ya usajili kwa mwaka ujao.
Kikosi
cha Luis Enrique bado kinatumikia kifungo cha kutosajili walichopewa
na FIFA baada ya kuvunja sheria za uhamisho kwa wachezaji wenye umri
chini ya miaka 18.
Kwa
mwaka 2015 Barcelona hawatakiwi kusaini mchezaji yeyote, lakini Mata
ambaye hana uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza cha Van Gaal
anahusishwa kujiunga na miamba hiyo ya Nou Camp, kwa mujibu wa gazeti la
Hispania la Mundo Deportivo.
0 maoni:
Post a Comment