Feb 14, 2015

PELLEGRINI: HATUMTEGEMEI YAYA

 
Mkufunzi wa Manchester United Manuel Pelegrini ana matumaini kwamba Manchester City inaweza kupambana ili kushinda taji la ligi kuu nchini Uingereza bila nyota wake Yaya Toure.
City haijashinda mechi yoyote ya ligi ya EPL tangu Toure aelekee Afrika katika michuano ya mataifa ya Afrika.
''Ni mchezaji muhimu sana na ni muhimu kwa yeye kurudi kikosini.Lakini hatutegemei mchezaji mmoja,lazima tushinde bila yeye'',.
City iko katika nafasi ya pili ikiwa nyuma ya Chelsea kwa pointi saba na hawajashinda katika mechi zote tano za ligi walizocheza,Hatahivyo Pelegrini anasema kuwa wanawaza kuhimili presha hiyo.

0 maoni:

Post a Comment