Fans wa muziki ni mashuhuda wa Collabo kali ambazo staa wa Nigeria, DAVIDO
ameshiriki na kuzifanya kuwa nyimbo kubwa Afrika na Duniani, sikuwahi
kusikia juu ya kiwango cha pesa ambacho analipwa ili kufanya collabo,
unaweza kuhisi anahitaji pesa kiasi gani ili afanye collabo yoyote?
Kwenye moja ya interview alizofanyiwa hivi karibuni Davido amesema anafanya muziki kwa sababu anaupenda, haitaji malipo yoyote kutoka kwa msanii ambaye anafanya naye Collabo, hakumbuki kama aliwahi kuhitaji malipo kwa ajili ya kushirikishwa kwenye ngoma yoyote.
“I
don’t charge for collabos, and I don’t think I have in the past. The
truth is I love music and I just do it out of the love. So, I do it for
free”– Davido.
Mbongo Fleva wetu DIAMOND PLATNUMZ ni mmoja ya mastaa ambao walipata nafasi kufanya collabo na DAVIDO na ikawa hit kubwa Afrika 2014.
0 maoni:
Post a Comment