Feb 14, 2015

SCHOLES ANENA

 
Aliyekuwa kiungo wa kati wa kilabu ya Manchester United Paul Scholes amesema kuwa mtindo wa timu hiyo ni m'bovu na unaenda kinyume na utamaduni wa kilabu hiyo wa kushambulia.
Mkufunzi Luois Van Gaal ameutetea mtindo huo baada ya kocha wa West Ham Sam Allardyce kuiita timu hiyo ''Long Ball United'' akiashiria mtindo wa pasi ndefu wa timu hiyo.
Scholes aliandika katika gazeti la independent nchini Uingereza :''kwa sasa ninashindwa kufurahia mechi za Man United''.
''Mara nyengine mtindo unotumiwa haufai''.
''Ukitaka kushinda wapinzani wako ni lazima ufanye mashambulizi na ili kufanikisha hilo lazima ujue kwamba pia kuna hatari yake''.
''Lakini ni wachezaji wachache katika timu hiyo ambao wako tayari kuwa jasiri."aliongezea Scholes.

0 maoni:

Post a Comment