Kocha Mkuu wa Azam FC, Joseph Omog, raia wa Cameroon, anatarajiwa
kuweka rekodi atakapoiongoza timu yake hiyo kuvaana na mabingwa wa Sudan, El
Merreikh katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi jijini Dar.
Kocha huyo ataingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kwa kuwa kocha wa
kwanza kuiongoza timu hiyo kucheza mchezo wa ligi hiyo inayosimamiwa na
Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
Msimu uliopita Azam ilishiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho,
lakini msimu huu wamepata nafasi hiyo baada ya kufanikiwa kubeba ubingwa wa
Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
Kocha huyo anaiongoza Azam kwa msimu wa pili baada ya kuanza kuinoa
timu hiyo msimu uliopita akichukua nafasi ya Stewart Hall, raia wa Uingereza.
0 maoni:
Post a Comment