Kiungo mwenye kazi wa Yanga, Simon Msuva, naye hakuwa nyuma kuelekea
katika mchezo huo baada ya kufunguka kwa kusema kuwa wapinzani wao BDF XI hao lazima wajipange kwa kuwa
yupo fiti.
Yanga inashuka dimbani
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwavaa BDF XI ya Botswana katika
mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.
“Tumejipanga vizuri, lengo letu ni kuhakikisha
tunanza kwa kasi kisha kuwamaliza mapema kwa kuwa nia yetu wote ni kusonga
hatua inayofuata ya michuano hiyo,” alisema Msuva.
Yanga italazimika kushinda
na ikiwezekana kwa mabao mengi zaidi ili kuhakikisha wanajiweka katika
mazingira mazuri kabla ya mechi ya marudiano.
0 maoni:
Post a Comment