Aggrey Morris (Kushoto)
Na Bertha Lumala
Utovu wa nidhamu wa wachezaji George Michael, Aggrey Morris na Juma Nyosso huenda ukawaponza kwa kupewa adhabu kali na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Kwa nini?
Muda mfupi uliopita mtandao huu umepata taarifa kwamba Kamati ya Nidhamu ya TFF, inaendelea na kikao cha dharura jijini Dar es Salaam kupitia malalamiko yaliyowasilishwa na klabu mbalimbali za Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza.
Januari 17 mfungaji bora wa VPL msimu uliopita, Mrundi Amisi
Tambwe alikabwa koo na beki George Michael wa Ruvu Shooting wakati wa
mechi yao ya raundi ya 11 ya ligi hiyo msimu huu waliyotoka suluhu.Utovu wa nidhamu wa wachezaji George Michael, Aggrey Morris na Juma Nyosso huenda ukawaponza kwa kupewa adhabu kali na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Kwa nini?
Muda mfupi uliopita mtandao huu umepata taarifa kwamba Kamati ya Nidhamu ya TFF, inaendelea na kikao cha dharura jijini Dar es Salaam kupitia malalamiko yaliyowasilishwa na klabu mbalimbali za Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza.
Beki wa kati Aggrey Morris wa Azam FC, alimpiga kiwiko kiungo mshambuliaji wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi wakati wa mechi yao ya raundi ya 12 ya VPL msimu huu iliyomalizika kwa sare ya bao moja kwenye Uwanja wa Taifa Januari 24. Baada ya kupigwa, Okwi alipoteza fahamu na kulazimika kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Siku nne baada ya tukio la Okwi, beki na aliyekuwa nahodha wa Mbeya City FC katika mechi ya kiporo ya raundi ya 10 ya ligi hiyo msimu huu dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Juma Nyosso alifanya kitendo cha udhalilishaji kwa kumpapasa makalio mshambuliaji Elias Maguli wa Simba.
Matukio yote matatu ambayo yanamtoa mchezaji moja kwa moja uwanjani kwa kuoneshwa kadi nyekundu kwa mujibu wa Sheria Namba 12 ya Soka (Makosa na Tabia Mbaya), hayakuonwa na marefa wa mechi husika.
Hata hivyo, viongozi wa Simba SC na Yanga SC wameshawasilisha malalamiko TFF kuhusu matukio hayo ambayo muda wowote kuanzia kesho adhabu zake zitaanikwa na TFF.
Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura amethibitisha kufanyika kikao cha Kamati ya Nidhamu leo lakini hakutaka kueleza kwa kina yanayojadiliwa katika kikao hicho.
Timu ya Friends Rangers ya Dar es Salaam inayoshiriki FDL msimu huu ikiwa Kundi A, huenda ikakumbwa na adhabu kubwa zaidi kwa kugomea mechi na baadhi ya wachezaji kumtwanga kwa mateke na ngumi refa wa kati wa mechi yake iliyopita dhidi ya Majimaji FC mjini Songea.
Majimaji FC walifunga bao la pili kwa mkono, goli ambalo liliwakwaza zaidi wachezaji wa Friends ambayo imekata rufaa Majimaji FC kupewa pointi tatu za mezani na mabao matatu na TFF ilhali mechi ilichezwa uwanja ukiwa umejaa maji.
0 maoni:
Post a Comment