Feb 4, 2015

ETO'O AANZA MATATIZO NA KOCHA SAMPODORIA

Etoo 2Ikiwa imepita wiki moja tu tangu asajiliwe na klabu ya Italia ya Sampdoria, mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto’o ameripotiwa kuwa kwenye utata wa kutaka kuihama klabu hiyo baada ya kutoelewana na kocha wake.

Kilichotokea ni kwamba Eto’o aliingia kwenye matatizo na kocha Sinisa Mihaijlovic baada ya kocha huyo kumtaka afanye mazoezi ya ziada baada ya mchezo ambao Sampdoria ilifungwa 5-1 na timu ya Torino katika muendelezo wa
ligi ya Italia maarufu kama Serie A.

Kwenye hiyo mechi Eto’o aliichezea klabu yake mpya kwa mara ya kwanza baada ya kuingia akitokea benchi kwenye dakika ya 71 japo uwepo wake haukuweza kuiokoa timu yake na kipigo ilichokipata toka kwa Torino .

Eto’o na kocha wake walifanya kikao cha dharura kuzungumzia kilichotokea baada ya mshambuliaji huyo kuamua kuondoka na kwenda Milan ambako familia yake ipo.
Inasemekana kuwa uhusiano kati ya Eto’o na kocha wake umefikia hatua mbaya kiasi cha klabu hiyo kuwa na wazo la kuvunja mkataba wake wamiaka miwili baada ya kusaini ndani ya wiki moja tu akitokea Everton.
Viongozi wa klabu hiyo ya Sampdoria wamekataa kuzungumzia tukio hilo wakisisitiza kuwa eto’o alikosa mazoezi kwa sababu zake binafasi lakini kocha anasema ‘Club ndio itajua nini cha kufanya ila kwangu mimi mchezaji anapofanya kitu kama hiki ni amenikosea heshima na kunidharau mimi na wafanyakazi wengine, aliondoka mazoezini bila kuniaga au kuomba ruhusa na hakurudi, sijamuona kuanzia asubuhi na sijaongea nae

0 maoni:

Post a Comment