Feb 4, 2015

SALA KWA MESSI, ISIHAKA WAKACHEZE REAL MADRID

 
Endapo watafanikiwa kucheza timu ya vijana ya klabu tajiri duniani, Real Madrid ya Uhispania, basi itakuwa ni habari njema kwa soka la Tanzania, ambayo wachezaji wake kadhaa wamekuwa wakifeli majaribio ya kucheza soka la kulipwa ughaibuni, hasa nchi za Ulaya katika miaka ya nyuma.
Kufuatia tetesi za kutakiwa kwenda kufanya majaribio Real Madrid, mashabiki wa soka wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam wamewaombea wachezaji wao kila la kheri katika majaribio yao ili waweze kusakata kabumbu Ulaya.

Haruna Hamisi, mmoja wa mashabiki na mwanachama wa Simba amesema beki wa kati wa klabu hiyo, Hassan Isihaka na straika Ramadhan Singano anayejulikana kama "Messi" kwa jina la uwanjani wana uwezo wa kucheza soka la kulipwa.

‘Vipaji tunavyo, ila vinakosa nafasi na kuharibiwa na mfumo wetu mbaya wa kutolea wachezaji wakiwa bado wadogo”, alisema Hamisi.
Emmanuel Temaeli, shabiki mwingine amesema endapo watafanikiwa, basi itakuwa faida si tu kwa Simba, bali taifa zima.

“Tukiwa na wachezaji wengi wanaocheza soka nje, tutakuwa na timu ya taifa imara kwa ajili ya michuano mbalimbali kama vile ya Mataifa ya Afrika na michuano ya kufuzu kucheza kombe la dunia”, alisema Temaeli.

Taarifa zinasema kuwa klabu ya Real Madrid ya Hispania, ambayo maofisa wake wamekuja nchini kuingia ubia na shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) kujenga kijiji cha michezo kwa ajili ya kulea wachezaji vijana kitakachosimamiwa na klabu hiyo ya Cristiano Ronaldo, wameomba CD (video) ili wawafanyie tathmini kupitia mechi walizocheza hivi karibuni.

Mabosi hao wamevutiwa na wachezaji hao vijana baada ya kuwaona katika mechi ya ligi kuu wakati Simba ilipocheza na klabu tajiri ya Azam na kutoka sare ya 1-1 majuma mawili yaliyopita.
Wachezaji kadha wa Tanzania wamefanikiwa kufanya majaribio kucheza nje bila mafanikio akiwemo mshambuliaji machachari, Mrisho Ngasa (anayecheza Yanga hivi sasa) aliyekwenda kufanya majaribio klabu ya West Ham ya Uingereza mwaka 2009 ikiwa chini ya kocha Gianfranco Zola.

Hivi karibuni, CSKA ya Urusi imemchukua mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na mchezaji wa klabu tajiri barani Afrika ya TP Mazembe ya Congo (DRC), Mbwana Samatta kwa ajili ya majaribio na tetesi zinasema mabosi wa timu wamevutiwa naye licha ya kuendelea kumjaribu

0 maoni:

Post a Comment