KLABU
ya West Ham imepigwa faini ya Pauni 71,000 na FIFA baada ya kumtumia
Diafra Sakho katika mechi ya Kombe la FA siku 18 tangu ajitoe kikosi cha
Senegal kilichocheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Sakho
alifunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 Uwanja wa Ashton Gate dhidi ya
Bristol City na bodi hiyo ya soka duniani ikaanza kufanya uchunguzi
kama walivunja sheria za majukumu ya kimataifa ya mchezaji.
The
Hammers walikanusha kufanya jambo lolote baya, wakisema mchezaji huyo
alikuwa ana maumivu ya mgongo wakati anaitwa Senegal na akashindwa
kujiunga na kikosi, lakini haikuwasaidia kuepuka rungu la FIFA.
+6
West Ham imeadhibiwa kwa kumchezesha Sakho aliyegoma kujiunga na timu yake ya taifa
Senegal ilikasirishwa na kitendo cha Sakho kuichezea West Ham saa 48 baada ya kutolewa kwao kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika.
0 maoni:
Post a Comment