KLABU ya Manchester United
imetinga Raundi ya Tano ya Kombe la FA baada ya ushindi wa mabao 3-0
Cambridge United Uwanja wa Old Trafford.
Timu ya kocha Mholanzi Louis Van Gaal iliyolazimishwa sare katika mchezo wa kwanza na wapinzani wao hao ugenini, jana ilikuwa tofauti katika mchezo wa pili wa Raundi ya Nne.

Juan Mata alianza kuwafungia bao la
kwanza Mashetani Wekundu dakika ya 25, kabla ya Marcos Rojo kufunga la
pili dakika ya 32 na James Wilson kumalizia la tatu dakika ya 73.
Sasa, Man United itasafiri kuwafuata Preston North End katika Raundi ya Tano Jumatatu ya Februari 16, mwaka huu.

Kikosi
cha Man Utd jana kilikuwa: De Gea, McNair, Smalling, Evans, Rojo/Young
dk81, Blind, Rooney, Di Maria/Herrera dk71, Mata, Van Persie/Wilson dk66
na Fellaini.
Cambridge Utd: Dunn, Tait, Nelson/Miller dk87, Coulson, Greg Taylor, Donaldson, McGeehan, Champion, Chadwick/Morrissey dk51, Elliott na Simpson/KaiKai dk61.

0 maoni:
Post a Comment