Baada ya kufanikiwa kuipa ushindi wa mabao 2-1
klabu yake ya Simba mbele ya JKT Ruvu Jumamosi iliyopita, mshambuliaji wa klabu
hiyo, Mganda, Danny Sserunkuma, ameweka rekodi ndani ya klabu hiyo ya kuwa
mchezaji pekee aliyepachika bao la mapema zaidi katika mechi za ligi kuu msimu
huu.
Sserunkuma ambaye alisajiliwa na Simba katika
usajili wa dirisha dogo msimu huu, ameshaichezea klabu hiyo mechi nne na
kufanikiwa kupachika mabao matatu, alifunga moja dhidi ya Ndanda na mawili
Jumamosi iliyopita kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar, Simba walionekana wazi kuupania ili kuibuka na ushindi, kwani
walianza kuwashambulia wapinzani wao kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la
kwanza katika dakika ya pili kupitia kwa mshambuliaji huyo Mganda.
0 maoni:
Post a Comment