Stori: CHAMPIONI
Beki mkongwe wa Mbeya City,
Juma Said Nyosso, amekubali kuwa kitendo alichomfanyia mshambuliaji wa Simba, Elias
Maguri na kuonyesha na gazeti la Championi si sahihi, si cha kiungwana na
anajuta kupita kiasi.
Kutokana na maumivu ya moyo
anayoyapata kutokana na kushiriki katika kitendo hicho, Nyosso amefanya mambo
mawili, kwanza ni kumpigia simu Maguri na pili kupiga katika ofisi za gazeti
hili.
Nyosso amesema alianza
kupiga simu kwa Maguri na kumuomba radhi akimueleza namna anavyojisikia vibaya
kutokana na kitendo hicho alichoona si sahihi.
Gazeti la Championi
linaloongoza kwa michezo nchini, lilichapisha picha zile zilizoonyesha Nyosso
akimtendea vitendo hivyo visivyo vya kiungwana wakati Simba
Akizungumza na Championi
Jumatano, Nyosso ambaye ni beki wa zamani wa Simba, alisema kuwa kwa sasa hana
tena amani kutokana na kitendo hicho alichomfanyia Maguri na amekuwa akitumia
muda mwingi kujikosoa mwenye bila
kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.
“Pamoja na hali hiyo nawaomba viongozi wangu wa Mbeya City na
wadau wa soka hapa nchini na duniani kote wanisamehe juu hilo, hakika halikuwa
kusudio langu kumdhalilisha Maguri.
“Nikiwa kama binadamu
wengine kusema kweli najisikia vibaya na ndiyo maana nimechukua uamuzi huu
ambao binafsi nauona kuwa ni wa busara kwa kumtafuta Maguri ili kumuomba radhi kwa
kitendo hicho nilichomfanyia.
“Nimetafuta namba yake,
halafu nimejitahidi kumpigia simu yake ya mkononi na kuzungumza naye kwa takribani
dakika mbili hivi. Lakini hakuonyesha dalili zozote za kunielewa nilichokuwa
nikimwambia.
“Kutokana na hali hiyo imebidi nitumiea njia hii ya
kuzungumza na Championi ili kumwomba msamaha yeye pamoja na viongozi klabu yake
ya Simba na klabu yangu Mbeya City, wanisamehe kwa kitendo kile.
“Kusema kweli nimejifunza
na sitorudia tena kufanya kitendo kama hicho kwa mchezaji yoyote yule kwani
hivi sasa najutia na ninajiona mkosefu mbele ya jamii. Nimefanya kosa hivyo
nahitaji kusamehewa,” alisema Nyosso.
Gazeti hili lilifanya kazi
ya kumtafuta Maguri ili kujua kama kweli aliwasiliana na Nyosso na alikubali
ombi la kumsamehe.
“Sijaongea naye na wala sihitaji kuzungumza naye kwa sababu
kitendo alichonifanyia kimenidhalilisha mbele ya ndugu zangu, rafiki zangu
pamoja na jamii yangu kwa ujumla.
“Kuna mtu alipingia simu
sijui kama alikuwa ni yeye akitaka nimsamehe, lakini nilimkatalia kwani wakati
alikuwa akifanya hivyo hakujua kama alikuwa ananidhalilisha?” alihoji Maguri.
“Kama kuna hatua za
kuchukuliwa basi atachukuliwa ili liwe fundisho kwa wachezaji wengine wenye
tabia kama za kwake ila kusema kweli kwa sasa siwezi kufanya hivyo,” alisema
Maguri ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Ruvu Shooting.
Nyosso amekuwa mmoja wa
wachezaji wa kwanza kuomba radhi baada ya kugundua kosa lake. Lakini Maguri
ameshikilia msimamo kutokana na kuumizwa na jambo hilo.
0 maoni:
Post a Comment