Feb 1, 2015

ALICHOSEMA BEN POL KUHUSU NYIMBO YA SOPHIA

 Star wa muziki wa R&B hapa Bongo, Ben Pol ametoa ya moyoni kuwa kwa namna flani, ngoma yake mpya ya SOPHIA ni rekodi ambayo ameifanya maalum kwaajili ya mtu wake wa karibu sana.


 

Ben Pol

Pol amesema kuwa mambo yakifanikiwa kuwa rasmi atamuweka wazi kwa watanzania ili wajue.
Ben ambaye katika ngoma hii ndani yake pia ameelezea uzuri wa mji wa Dodoma ambapo ndipo anapotokea, amesema kuwa ana imani mambo yatakuwa vizuri hapo baadaye kwaajili ya kumleta mwanadada huyo mbele ya mashabiki zake, ikiwa sasa mambo yao yanaendelea chini ya kapeti tu.

0 maoni:

Post a Comment