Feb 1, 2015

WENYEJI WAPITA KWA MBINDE AFCON

Wenyeji Equatorial Guinea wametoka nyuma kwa goli 1-0 na kushinda goli 2-1 dhidi ya Tunisia hivyo kufuzu nusu fainali ya kombe la Mataifa Afrika 2015. Shukrani kwa mfungaji wa mabao yote mawili kwa mpira wa adhabu Javier Balboa usiku wa jana katika mchezo uliodumu kwa dakika 120.
Balboa alianza kufunga kwa penalti ya utata dakika ya 90 kusawazisha bao la Tunisia lililo fungwa na Ahmed Akaichi dakika ya 70 na baadae akafunga bao la pili kwa mpira wa adhabu dakika ya 101 na kuipeleka Equatorial Guinea nusu fainali.

Mchezaji Javier balboa akishangilia katika moja ya mechi zao.

Kwa matokeo hayo EG itakutana na mshindi kati ya Ghana na Guinea watakao cheza leo jumapili

0 maoni:

Post a Comment