Manchester United imefanikiwa
kulipa kisasi dhidi ya Leicester City kufuatia kuibuka na ushindi wa
mabao 3-1 katika uwanja wa Old Trafford. Robbin Van Persie na Radamel
Falcao walifunga katika dakika za 27 na 32 kabla ya Wes Morgan kujifunga
dakika ya 44 na kufanya vijana wa Luis Van Gaal kuwa mbele kwa mabao
3-0 kufikia nusu ya mchezo. Marcin Wasilewski
aliwafungia wageni bao la
kufutia machozi katika dakika ya mwisho ya mchezo.
Ikicheza katika uwanja wa
nyumbani, Britania, Stoke City iliichapa QPR kwa mabao 3-1. Jonathan
Walters alifunga mara mbili katika dakika za 21 na 24 kabla ya Niko
Kranjcar kuiwafungia wageni goli la kufutia machozi katika dakika ya 36.
Walters alifunga ‘ hat-trick’ baada ya kuzamisha bao la tatu dakika ya
mwisho ya mchezo.
Mshambulizi Jermaine Defoe
alifunga bao lake la kwanza tangu alipojiunga na Sunderland akitokea
Toronto ya Marekani. ‘ Black Cats’ walichomoza na ushindi wa mabao 2-0
katika uwanja wa Stadium of Right dhidi ya Burnley. Connor Wickham
aliwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 20 kabla ya Defoe kufunga
lingine dakika 14 baadae.
IKicheza katika uwanja wa
nyumbani The Hawthorns timu ya West Brom ilivurumishwa mabao 3-0 na
Tottenham Hotspur. Cristian Eriksen aliifungia Spurs bao la uongozi
dakika ya 6 kabla ya Harry Kane kufunga mara mbili katika dakika za 15
na 64 alipofunga kwa mkwaju wa penalti.
0 maoni:
Post a Comment