Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imeendelea hii leo kwa michezo miwili iliyopigwa jijini Dar-es-salaam pamoja na huko mkoani pwani ambako timu nne zilikuwa viwanjani zikisaka pointi tatu muhimu .
Jijini Dar-es-salaam uwnaja wa taifa ulishuhudia mchezo kati ya mabingwa wa zamani wa ligi hiyo Dar-es-slaam Young Africans dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu ya Ndanda Fc toka Mtwara .
Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa kuashiria mchezo huo kumalizika hakukuwa na timu iliyoweza kumtambia mwenzie baada ya timu hizo mbili kutoka sare ya bila kufungana .
Hata hivyo Yanga watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuondoka na ushindi baada ya kutengeneza nafasi kadhaa za wazi ambazo kama washambuliaji wake wangekuwa makini basi Yanga ingeweza kushinda .
Katika mchezo mwingine uliopigwa huko mkoani Pwani kwenye uwanja wa Mabatini wenyeji Ruvu Shooting waliwafunga Stand United kwa mabao mawili kwa moja .
Ruvu Shooting walifunga mabao yao kupitia kwa Juma Mpakala kwenye dakika ya tano ya mchezo huku bao la ushindi likija kupitia kwa Yahya Tumbo kwneye dakika ya 89 na Stand United wakafunga kupitia kwa Hamis Thabit .
Matokeo ya michezo ya leo yanawafanya Yanga washindwe kuwafikia Azam Fc kwenye kilele cha msimamo wa ligi ya Tanzania Bara ambapo hadi sasa wana pointi 19 wakiwa wamezidiwa kwa pointi mbili na Azam wenye pointi 21 .
0 maoni:
Post a Comment