Feb 1, 2015

MADRID BILA RONALDO INAWEZEKANA


(null)
Ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga imeendelea tena jioni ya leo kwa mchezo ambao ulivihusisha vilabu vya Real Madrid na Real Sociedad.
Mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu, ulikuwa ndio wa kwanza kwa kocha wa zamani wa Man United – David Moyes katika uwanja huo.
Huku wakicheza bila mshambuliaji wao tegemeo Cristiano Ronaldo ambaye amesimamishwa mechi mbili – Real Madrid leo wameiadhibu Sociedad magoli 4-1.
Sociedad ndio walioanza kuziona nyavu za Madrid katika dakika ya kwanza tu ya mchezo lakini dakika mbili baadae Real walisawazisha kupitia James Rodriguez.
Ramos aliongeza lingine dakika ya 36, na Benzema akashindilia misumari ya mwisho dakika ya 51 na 76.

0 maoni:

Post a Comment