Tetesi kuhusu mustakabali wa kipa Mhisapnia David De Gea ndani ya klabu ya Manchester United zimezidi kuibuka ambapo kila siku ameendelea kuhusishwa na kujiunga na mabingwa wa ulaya Real Madrid ambao wametajwa kuwa na mpango wa kumsajili kipa huyo .
Taarifa toka England na Hispania zinasema kuwa wawakilishi wa kipa huyo wanataka kuwepo na kipengele kinachoruhusu kipa huyo kuuzwa ndani ya mkataba mpya ambao anatarajiwa kuusaini .
De Gea amebakiza miezi 18 kabla ya kumaliza mkataba wake wa sasa na United na klabu hiyo imekuwa katika mkakakati wa kuhakikisha kipa huyo anasaini mkataba mpya ambao una maslahi yaliyoboreshwa tofauti na mkataba wake wa sasa .
Katika kuhakikisha kipa huyo anabaki United , timu hiyo imejiandaa kumfanya De Gea kuwa kipa anayelipwa fedha nyingi kuliko wote duniani kwa mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki lakini wawakilishi wa kipa huyo wamekuwa kikwazo kwa harakati hizi za United .
De Gea kwa mbali amekuwa mchezaji bora kwa timu yake ambapo kwenye michezo kadhaa amekuwa akiikoa huku akionyesha kiwango cha juu hali ambayo imemfanya atajwe kuwa moja ya makipa bora duniani .
Real Madrid kwa muda mrefu wamekuwa na shauku ya kumsajili Mhispania huyu ambaye kwa upande mwingine ameonyesha dhamira ya kurudi nyumbani kwao jijini Madrid .
Kitendo cha United kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdez kimeongeza fununu za kuondoka kwa De Gea na mpaka sasa bado uongozi wa United unahaha kuhakikisha unambakiza kipa huyo
0 maoni:
Post a Comment