Kocha
Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema mechi ya leo dhidi ya Ndanda
ni sahihi kwao kujirekebisha na kuyafanyia kazi waliyojifunza kwa zaidi
ya siku 7.
Yanga inaikaribisha Ndanda FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo.
Pluijm raia wa Uholanzi amesema ni wakati mwafaka kuyafanyia kazi mambo walioyokosea katika mechi iliyopita.
"Ushindi ndiyo jambo muhimu, lakini hatuwezi kushinda kama hatujayafanyia marekebisho matatizo yetu.
"Ninaamini wachezaji watafanya hivyo na itakuwa njia ya kuendelea kufanya vizuri zaidi," alisema.
Pluijm
amesema anaamini ana kikosi kizuri kinachoweza kuifumua Ndanda lakini
lazima nafasi zitakazopatikana zitumiwe kwa asilimia angalau 70.
Yanga imekuwa ikiongoza kwa kutengeneza nafasi nyingi, pia kupoteza nyingi katika Ligi Kuu Bara.
0 maoni:
Post a Comment