Mabao mawili aliyofunga Danny Sserunkuma
wakati Simba ikiimaliza Ruvu JKT kwa mabao 2-1 leo, amezawadiwa Kocha Goran
Kopunovic.
Wachezaji Simba wameamua kumzadia kocha huyo
mabao hayo kwa kuwa leo ni siku yake ya kuzaliwa, anafikisha miaka 48.
Kabla ya mchezo huo, Kopunovic aliwaomba
wachezaji hao kumzawadia kitu kizuri kwa ajili ya sikukuu yake ya kuzaliwa.
“Kweli kocha aliwaambia anaomba msaada wao,
aliwaambia angependa kusherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa na amani.
“Hivyo aliwaomba kuifunga Ruvu JKT ili
Wanasimba wafurahi naye awe na amani hiyo kesho.
“Kweli utaona wachezaji wamejituma sana
licha ya mechi kubwa ngumu na mwisho wamefanikiwa kushinda na baada ya hapo
wamemzawadia mabao hayo mawili ya Sserunkuma,” kilieleza chanzo.
Huo ni mchezo wa tatu wa Kopunovic akiwa na Simba katika Ligi Kuu Bara na amefanikiwa kushinda mechi mbili na kupoteza mmoja.
0 maoni:
Post a Comment