Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika imeendelea hii leo kwa kushuhudia mchezo mmoja wa hatua ya robo fainali ukizikutanisha Ghana pamoja na Guinea .
Katika Mchezo huo Ghana walifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali wakiwafunga Guinea kwa mabao matatu bila .
Ghana walianza kazi mapema wakifunga bao mapema kwenye dakika ya nne kupitia kwa winga Christian Atsu .
Black Stars walipata bao la pili kwenye kipindi cha kwanza mfungaji akiwa Kwessi Appiah bao ambalo liliua matumaini ya Guinea .
Mwanzoni mwa kipindi cha pili Ghana walifunga bao la tatu mfungaji akiwa Christian Atsu tena na kuikatia timu yake tiketi ya kufuzu hatua ya nusu fainali .
Nafasi ya mwisho kwenye hatua ya nusu fainali itafahamika saa chache zijazo wakati mchezo wa mwisho wa roo fainali utakaowakutanisha Ivory Coast na Algeria utakapopigwa .
Hadi sasa timu tatu tayari zimefuzu hatua ya nusu fainali nazo ni wenyeji Equatoarial Guinea , Ghana pamoja na Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo .
0 maoni:
Post a Comment