Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga klabu ya Simba faini ya sh.
milioni tatu kutokana na timu yake kuvaa jezi ambazo hazikuwa na nembo
ya mdhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya Vodacom wakati wa mechi yao dhidi ya
Kagera Sugar.
Mechi hiyo namba 50 ya Ligi Kuu ya Vodacom ilichezwa Desemba 26 mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Adhabu
hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 13(7) ya Ligi Kuu inayotaka
klabu kuheshimu masharti ya udhamini wa Ligi Kuu kwenye mechi zake.
Nayo
Polisi Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya
28(4) kwa kusababisha mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati yake na
Toto Africans iliyochezwa Januari 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza kuvurugika.
Kutokana
na mchezo huo kuvurugika, Toto Africans imepewa ushindi wa pointi tatu
na mabao matatu. Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia kanuni ya 28(1)
inayotawala ligi hiyo.
0 maoni:
Post a Comment