Dully Sykes
ni mmoja ya mastaa ambao wamekuwa kwenye njia ya safari ya Bongo Fleva
kwa muda, huenda mapenzi ya baba yake mzazi kwenye muziki kulifanya Dully awe zaidi ya msanii mwenye kipaji cha kuimba peke yake.
Leo FEB 15 majonzi kwa ndugu, jamaa na watu wa karibu na familia ya mzee Abby Sykes, baba mzazi wa Dully ambaye kwa taarifa niliyoipata muda mfupi uliopita ni kwamba mzee Abby Sykes amefariki.
Wengi tulimfahamu kutokana na ukaribu wake na Bongo Fleva, aliwahi kuonekana kwenye video za mastaa kadhaa, ikiwemo video ya Daz Baba “Usiku Huu” pamoja na video ya ROMA “Kidole cha Mwisho Juu“.
Hivi ndivyo alivyo andika Dully Sykes "KWAHERI BABA YANGU MPENDWA.........KIPENZI CHANGU ...........RAFIKI YANGU............MTANI WANGU .........MWALIMU WANGU..............DAMU YANGU.........KIPENZI CHA WATU..........BABA YANGU MPENZI.........SIAMINI EBBY WANGU!!!!! NAKUPENDA NA NTAKUPENDA MPAKA MWISHO WA MAISHA YANGU R.I.P DAD 1952-2015 Ameandika Dully.
0 maoni:
Post a Comment