Feb 15, 2015

FA CUP: ADAM LALLAN ATUPIA LA USHINDI LIVERPOOL WAKING’ARA 2-1


article-2953713-25AE88B700000578-556_964x385

LIVERPOOL imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika mechi ya raundi ya tano ya kombe la FA.
Palace walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 16′ kupitia kwa Fraizer Campbell kabla ya Daniel Sturridge kuisawazishia Liverpool katika dakika 50′.
Dakika ya 58′ Adam Lallan aliwafungia majogoo wa jiji bao la pili na la ushindi.
Katika mechi nyingine, Derby County ikiwa nyumbani imechapwa mabao 2-1 na Reading.
Blackburn Rovers imeichapa 4-1 Stoke City na West Brom imeilaza 4-0 West Ham United.

0 maoni:

Post a Comment