WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC,
wameunguruma katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro baada ya
kuitandika mabao 2-0 Polisi Moro katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania
bara iliyomalizika jioni hii.
Bao la kwanza la kikosi hicho cha
Mserbia, Goran Kopunovic limefungwa na Ibrahim Hajib ‘Mido’ katika
dakika nya 14’ ya kipindi cha kwanza.
Hadi dakika 45’ za kipindi cha kwanza zinamalizika Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili Simba
waliendelea kulisakama lango la Polisi na katika dakika ya 63’ ya
kipindi hicho, Elius Maguli aliwanyanyua tena mashabiki wa Simba kwa
kuandika bao la pili na la ushindi.
Ushindi huo umeifanya Simba
ifikishe pointi 20 baada ya kushuka dimbani mara 14 na sasa inazipumulia
Yanga na Azam ambazo zipo juu kwa pointi 5 zaidi.
Kujua nafasi ya Simba katika msimamo tunasubiria matokeo ya Kagera Sugar na JKT Ruvu uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Kabla ya mechi ya leo, Polisi
Morogoro walikuwa nafasi ya tatu wakijikusanyia pointi 19 kibindoni,
wakifuatiwa na JKT Ruvu wenye pointi 19.
Kama JKT Ruvu wamefungwa, basi
Simba watapanda mpaka nafasi ya tatu nah ii itakuwa faraja kubwa kwa
Wana Msimbazi. Mtandao huu unafuatilia kwa umakini matokeo ya huko na
yakipatikana utajulishwa.
Azam wanaongoza katika msimamo
wakijikusanyia pointi 25 baada ya kushuka dimbani mara 13 sawa na Yanga
wenye pointi 25 kwa mechi 13 walizocheza, lakini wana Lambalamba wana
wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
0 maoni:
Post a Comment