FAINALI za Mataifa ya Afrika kwa
vijana chini ya umri wa miaka 17 zinaanza leo mjini Niamey, Niger,
wakati kesho Ivory Coast ikifungua dimba na Afrika Kusini, mechi ambayo
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa
Kamisaa.
Mechi za ufunguzi leo ni kati ya wenyeji Niger
dhidi ya Nigeria Saa 9:00 Alasiri kwa saa za huko na Saa 11:00 kwa Saa
za Afrika Mashariki, wakati mchezo wa pili utakuwa kati ya Guinea na
Zambia Saa 12:00 za huko na Saa 2:00 kwa saa za kwetu.
Mchezo wa Ivory na Afrika Kusini, utafuatiwa na mchezo kati ya Mali na Cameroon kesho.
Michuano hiyo ya U17 Afrika itaanza leo hadi Machi 2, mwaka huu na timu zitakazofanikiwa kutinga Nusu Fainali, moja kwa moja zitakuwa zimejikatia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia nchini Chile baadaye mwaka huu.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (katikati) akiongoza kikao cha kabla ya mechi baina ya Ivory Coast na Afrika Kusini leo katika hoteli ya Gaweye mjini Niamey, Niger |
Viongozi wa Afrika Kusini katika kikao cha kabla ya mechi na jezi zao |
Viongozi wa Ivory Coast katika kikao cha kabla ya mechi leo |
Mchezo wa Ivory na Afrika Kusini, utafuatiwa na mchezo kati ya Mali na Cameroon kesho.
Michuano hiyo ya U17 Afrika itaanza leo hadi Machi 2, mwaka huu na timu zitakazofanikiwa kutinga Nusu Fainali, moja kwa moja zitakuwa zimejikatia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia nchini Chile baadaye mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment