KAVUMBAGU AKISHANGILIA BAADA YA KUIFUNGIA BAO AZAM FC LEO DHIDI YA VIGOGO BARANI AFRIKA, EL MERREIKH YA SUDAN. |
Ingawa
ilionekana haitawezekana, Azam FC wamebadili mambo na kuonyesha katika
soka kweli linawezekana baada ya kuichapa El Merreikh ya Sudan kwa mabao
2-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Azam FC wameshinda mechi hiyo leo katika pambano tamu na la kuvutia katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.
Didier Kavumbagu ndiye alikuwa wa kwanza kuioatia Azam FC bao baada ya mabeki wa Wasudan hao kujichanganya.
Haikuwa
kazi lahisi kwa kuwa El Merreikh walikuwa wasumbufu na walicheza kwa
mipangilio na walionyesha kwamba wana kitu wanatafuta.
Nahodha wa Azam FC, John Bocco ambaye alitokea benchi kama ilivyo kawaida yake siku hizi, aliifungia Azam FC bao la pili.
Bocco
alifunga bao hilo kwa kichwa baada ya mpira wa kichwa kutua kichwani
mwa Kavumbagu, halafu ukawapita mabeki wa El Merreikh kabla ya kumkuta
mfungaji.
Kwa ushindi huo, Azam FC, inalazimika kwenda kuulinda ugenini wiki mbili zijazo ili iweze kusonga mbele.
0 maoni:
Post a Comment