Feb 15, 2015

SIMBA KAMILI KUIVAA POLISI MORO


okwi-na-simba-jifua
MJI wa Morogoro uko shwari kabisa mpaka muda huu! huku wadau wa soka wakisubiri mechi ya jioni uwanja wa Jamhuri baina ya Polisi Morogoro na Mnyama Simba.
Afisa habari wa Simba, Humphrey Nyasio ameuambia mtandao huu kuwa kikosi cha Simba kipo tayari kuchukua pointi tatu muhimu.
“Sisi tuko poa kabisa. Vijana wanasubiri muda ufike wakafanye kazi ya kuzichukua pointi tatu kutoka kwa Polisi Moro”. Amesema Nyasio.
Polisi nao wametamba kuizima Simba katika mechi ya leo.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Rishard Adolf amesema wanajua Simba wamejiandaa kuchukua pointi tatu, lakini mipango yao haitatimia kwasababu Polisi iko imara idara zote.
“Tumejiandaa vizuri, tuko tayari kwa mechi hii”. Amesema Adolf.
Mechi nyingine jioni ya leoinapigwa uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga ambapo Kagera Sugar wanachuana na JKT Ruvu.

0 maoni:

Post a Comment