Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, amemuomba radhi askari aliyemkimbilia na kwenda kumkumbatia dakika
chache baada ya kufunga bao katika mechi dhidi ya Coastal Union.
Cannavaro alifunga bao hilo katika dakika ya
11, Jumatano iliyopita na kufanya kitendo hicho ambacho kilikuwa gumzo.
Cannavaro
alisema alimuomba askari huyo msamaha muda mfupi baada ya mechi hiyo ambapo
aliamua kumfuata na kumueleza kuwa hakuwa na nia mbaya.
Cannavaro alisema anamshukuru askari huyo kwa
kukubali maombi yake ya msamaha aliyoyatoa kwani hakutarajia hali hiyo kutokea
kutokana na furaha aliyoipata baada ya kufunga bao hilo.
“Kiukweli nilifanya kosa kukimbia na kwenda
kumkumbatia askari wakati nashangilia bao nililolifunga, nilijikuta ghafla
nafanya kitendo kile bila kutarajia, sikukitarajia kabisa wala sikupanga iwe
hivyo.
“Baada ya mechi kumalizika nilimfuata
nikazungumza naye, pia walikuwepo baadhi ya viongozi wangu na wale wa polisi
niliwaomba radhi kwa kitendo hicho nilichokifanya,
nikashukuru wakanielewa na
kulimaliza tatizo hilo,” alisema CannavaroUSIKOSE KUFUATIIA WWW.HAJIBALOU.BLOGSPOT.COM KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI
0 maoni:
Post a Comment