TIMU ya Atletico Madrid imeitandika mabao 4-0 Real Madrid katika mchezo wa La Liga jioni ya leo.
Mwanasoka
Bora wa dunia, Cristiano Ronaldo alicheza kwa mara ya kwanza baada ya
kumaliza adhabu yake, lakii alitoka uwanjani anazomewa na mashabiki wa
wenyeji baada ya kipigo.
Kiungo
wa zamani wa Chelsea, Tiago alifunga bao la kwanza dakika ya 14, Saul
Niguez akafunga la pili dakika ya 18, kabla ya Antoine Griezmann kufunga
la tatu dakika ya 67 na Mario Mandzukic kufunga la nne dakika ya 89 kwa
pasi ya Fernando Torres.
Kikosi
cha Atletico Madrid kilikuwa; Moya, Juanfran, Miranda, Godin, Siqueira,
Tiago, Koke/Saul dk10/Garcia dk71, Gabi, Turan, Griezmann/Torres dk77
na Mandzukic.
Real
Madrid; Casillas, Coentrao, Nacho, Varane, Carvajal, Khedira/Jese dk46,
Kroos, Isco/Illaramendi dk68, Bale, Ronaldo na Benzema/Hernandez dk73.
Cristiano Ronaldo akiwa mnyonge baada ya Real Madrid baada ya Real kufungwa bao la pili katika kipigo cha 4-0 leo
0 maoni:
Post a Comment