Mchezaji wa zamani na kocha wa timu ya taifa ya
Rwanda ‘Amavubi’, Jean Marie Ntagwabira amezikwa juzi katika makaburi ya
kijeshi jijini Kigali, Rwanda.
WATOTO WA MAREHEMU WAKITOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO |
Mwezi
mmoja kabla ya kifo chake, Ntagwabira aliwaniwa na Simba lakini mwisho
nafasi yake akaitwaa Goran Kopunovic ambaye pia aliiambia SALEHJEMBE
kushitushwa na kifo chake.
NTAGWABIRA WAKATI WA UHAI WAKE. |
Mchezaji wa zamani na kocha wa timu ya taifa ya
Rwanda ‘Amavubi’, Jean Marie Ntagwabira amezikwa juzi katika makaburi ya
kijeshi jijini Kigali, Rwanda.
Ntagwabira ,41, amefariki dunia akiwa
anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu uliofanya ashindwe kupumua.
Mazishi yake yalihudhuriwa na maofisa mbalimbali
wa jeshi pamoja na wanamichezo mbalimbali wakiwemo makocha na wachezaji wa timu
ya APR.
Wakati wa mazishi yake, Rais wa Shirikisho la
Soka la Rwanda (Ferwafa), Vincent Nzamwita alitoa pole kwa wafiwa, wadau wote
wa soka la Rwanda pamoja na familia ya marehemu.
Lakini Shirikisho hilo pia likaahidi kuwasomesha
watoto wa marehemu kwa kiwango chote cha elimu watakachofikia.

0 maoni:
Post a Comment