Feb 7, 2015

JINAMIZI LA SARE LAENDELEA MSIMBAZI

COASTAL Union wamegoma kufungwa mechi ya pili mfululizo nyumbani, baada ya jioni ya leo kulazimisha sare ya 0-0 na Simba SC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba ilijaribu kutengeneza mashambulizi ya mipira ya kutokea pembeni, lakini washambuliaji wake Dan Sserunkuma na Elias Maguri walibanwa na walinzi wa Coastal.
 
Hali kadhalika Coastal nayo ilitengeza mashambulizi yake kadhaa, lakini washambuliaji wake Iker Obinna na Rama Salim walibanwa na mabeki wa Simba SC.
Kiungo wa Simba SC, Abdi Banda akipasua katikati ya wachezaji wa Coastal Union, Abdulhalim Humud kushoto na Godfrey Wambura kulia

Hakukuwa na mchezo wa kuvutia sana kutokana na timu zote kucheza mipira mirefu kwa kuhofia ubovu wa Uwanja wa Mkwakwani, lakini hakukuwa na kupamiana kama ilivyokuwa Jumatano Coastal ikifungwa 1-0 na Yanga SC. 
Refa wa mchezo Simon Mbelwa aliyesaidiwa na Abdallah Mkomwa na Frank Kombo wote wa Pwani, kwa kiasi kikubwa walijitabhidi kuumudu mchezo huo.
 
Kwa matokeo hayo, Coastal inafikisha pointi 18, wakati Simba SC inatimiza pointi 17.
Kikosi cha Coastal Union kilikuwa; Shaaban Kado, Mbwana Hamisi, Othman Tamim, Abdallah Mfuko/Hamad Juma dk59, Juma Lui, Abdulhalim Humud, Joseph Mahundi/Itubu Imbem dk86, Godfrey Wambura, Bright Ike Obinna/Mohammed Mtindi dk66, Hussein Sued na Rama Salim.  

Simba SC; Ivo Mapunda, Kessy Ramadhani, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Simon Sserunkuma/Messi dk79, Abdi Banda, Dan Sserunkuma/Ibrahim Hajibu dk88, Elias Maguri na Emmanuel Okwi.
Kipa wa Simba SC, Ivo Mapunda akidaka mpira leo
Kipa wa Coastal Union, Shaaban Kado akidaka mpira mbele ya beki wake, Tumba Swedi ambaye yuko mbele ya mshambuliaji wa Simba SC, Dan Sserunkuma

USIKOSE KUFUATILIA WWW.HAJIBALOU,BLOGSPORT.COM KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

0 maoni:

Post a Comment