Feb 7, 2015

PEDRO KUONDOKA BARCELONA


Klabu za Liverpool na Arsenal zote za nchini England huenda zikapigana vikumbo mwishoni mwa msimu huu, kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Hispania, Pedro Rodriguez ambaye yu njiani kuachana na FC Barcelona.

Arsenal na Liverpool zinatajwa kuingia katika mvurugano wa kumuwania mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, kufuatia mipango iliyobainika huko mjini Barcelona ambayo inabainisha huenda Pedro akatemwa mwishoni mwa msimu huu kutokana na mapendekezo ya meneja wa sasa Luis Enrique.
Hata hivyo mkataba mshambuliaji huyo unatarajia kufikia kikomo mwaka 2016, lakini FC Barcelona wanahofia kumpoteza bila ya kupata faida ya ada ya uhamisho endapo ataondoka kama mchezaji huru, hivyo wameona ni bora kumuingiza katika mfumo wa kumuuza mwishoni mwa msimu huu.

Padro amekua na mafanikio katika klabu ya Barcelona ambayo ameitumikia kwa muda wa miaka 11 sasa, ambapo ameshwatwaa mataji manne ya ligi ya nchini Hispania pamoja na mataji mawili ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, ila amekua na wakati mgumu kwa msimu huu kutokana na kutumika mara 20 kikosini.

0 maoni:

Post a Comment