MSHAMBULIAJI
wa Real Madrid, James Rodriguez juzi ameanza kutembelea magongo baada
ya kufanyiwa upasuaji wa goti la mguu wake wa na anatarajiwa kuwa nje
kwa miezi miwili.
Japokuwa
klabu yake haijasema atakuwa nje kwa muda gani, lakini taarifa za ndani
zinasema mchezaji huyo atakosekana kwa miezi miwili.
Rodriguez
aliumia goti baada ya kuifungia bao la kuongoza Real Madrid katika
ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa La Liga dhidi ya Sevilla Uwanja wa
Santiago Bernabeu na akatolewa kipindi cha kwanza baada ya madaktari
kusema kwamba ameumia sana.
James Rodriguez pichani baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Murcia
Nyota
huyo mwenye umri wa miaka 23, Rodriguez amefanikiwa kupata namba kwenye
kikosi cha kwanza Real chini ya kocha Carlo Ancelotti, baada tu ya
kusajiliwa msimu huu kufuatia kuifikisha timu yake ya taifa Colombia,
katika Robo Fainali Kombe la Dunia hadi kuibuka mfungaji bora.
Amecheza mechi 33 kati ya 36 za Real Madrid msimu huu, akifunga mabao 12 na kusaidia upatikanaji wa mabao 10 zaidi.
0 maoni:
Post a Comment