Kiungo Mkenya, Paul Raphael Kiongera ametishia kujiondoa mikononi mwa klabu ya Simba kama hakutakuwa na mabadiliko.
Kiongera ameliambia gazeti hili kuwa amechoshwa
na kile alichokiita ‘uswahili mwingi’ ambapo anadai kutolipwa fedha yoyote
tangu Desemba, mwaka jana.
Simba iliondoa jina la mchezaji huyo katika
usajili wake wa msimu huu licha ya kuwa na mkataba naye, ambapo ilisema
itaendelea kumlipa kama kawaida kwa kuwa itamhitaji baada ya kupona jeraha la
goti lililokuwa likimsumbua na kusababisha akatibiwe nchini India ambapo Simba
ndiyo iliyogharamia huduma zake.
Akizungumza kutoka jijini Nairobi, Kiongera amesema:
“Ni kweli nasubiri Februari hii iishe, nimalizane
nao kwa mujibu wa mkataba wetu, wao ndiyo watakuwa wamekiuka masharti
na wameuvunja.
“Naona Simba wananizingua tu. Ujue hawataki
kunipa mshahara wangu.”
Lakini Simba imesisitiza kwamba inamlipa fedha zake na hadai chochote.
Mwenyekiti wa
Usajili, Zacharia Hans Poppe, alisema: “Kweli Kiongera tuna dhamana ya kumlipa
na binafsi najua analipwa fedha zake na hakuna madai yoyote juu yetu. Sina
taarifa zozote juu ya yeye kutolipwa kwa kuwa mi najua analipwa kama kawaida,
vinginevyo aulizwe katibu.”
0 maoni:
Post a Comment