Feb 2, 2015

ALICHOSEMA SIMON MSUVA KUHUSU YANGA

 
 Simon Msuva wa Yanga kushoto akimtoka beki wa Mtivwa
 
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, amefunguka kuwa hakuna aliyejihakikishia namba katika timu hiyo, hivyo kila mmoja anacheza kuhakikisha anapata nafasi ya kuitumikia timu hiyo katika kiwango kizuri.

Msuva amefunguka kuwa, kwa jinsi ushindani uliokuwepo katika kikosi hicho, hakuna mchezaji hata mmoja aliyejihakikishia namba.

“Kila mmoja anahitaji kujituma ili kuweza kupata nafasi na hatimaye kufikia malengo ya kuisaidia timu yetu, hivyo hakuna mchezaji aliyejihakikishia namba.

“Moja ya malengo yangu ni kuona naisaidia timu yangu kuweza kufanya vizuri na hatimaye kufanikiwa kutwaa ubingwa,” alisema Msuva.

0 maoni:

Post a Comment