KOCHA wa Azam, Joseph Omog, amesema kiungo wake Frank Domayo ameonyesha kiwango cha juu na cha kushangaza ikiwa amecheza mechi chache tu baada ya kupona majeraha ya nyama za paja.
Domayo aliifungia Azam mabao yote mawili katika
sare ya 2-2 na Zesco ya Zambia juzi Jumamosi, lakini mbali ya hilo
alionyesha kiwango cha kuvutia kilichowashangaza wadau wengi wa soka
waliokuwepo uwanjani hapo.
Kiungo huyo ameanza kucheza mwezi uliopita baada ya kukaa nje kwa miezi sita tangu alipofanyiwa upasuaji Afrika Kusini.
Omog alisema hakutarajia kama Domayo angeweza
kurejea katika makali yake ndani ya muda mfupi kama ilivyokuwa lakini
bado anashindwa kumtumia kwa dakika zote 90 kwa hofu ya kumuumiza.
Katika hatua nyingine, kocha wa Zesco, George Lwandamina amesema
Azam wanahitaji kufanya marekebisho kidogo tu
katika kikosi chao ili waweze kufanya vizuri katika mashindano ya
kimataifa yanayowakabili.
Azam itacheza Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya
kwanza mwaka huu baada ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika miaka
miwili mfululizo.
0 maoni:
Post a Comment